Thursday, August 11, 2016

MAONESHO YA NANE NANE MWAKA 2016 KANDA YA KATI DODOMA.
Maonesho ya Nane Nane mwaka huu 2016 kanda ya kati yamefanyika viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma kwa kushirikisha Mikoa ya Dodoma na Singida.
Maonesho hayo ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama sherehe za Nane Nane yalianza tarehe 01-08/08/2016 sehemu mbalimbali nchini na kitaifa yalifanyika Mkoani Lindi.
Afisa kilimo (w) ndugu Funda alisema, Maonesho hayo kwa kanda ya kati yalikuwa ni mazuri na Wilaya ya Chemba ilishiriki kwa kiasi kikubwa kuanzia tarehe 01- 08/08/2016. Idara tatu zilishiriki kuwakilisha wilaya kwa kuonesha shughuli mbalimbali zikiwemo; vipando mbalimbali, bidhaa za mbegu zilizosindikwa, mifugo, huduma ya uzazi wa mpango, upimaji wa ukimwi n.k.
Afisa Kilimo (w) alisema, Wilaya ya Chemba imepata Mafanikio kwa kupata cheti cha Ushiriki pamoja na  Mfugaji wa ng’ombe Bw.Mohamedi Deketi alipata zawadi ya mfugaji bora wa ng’ombe (mtamba asiye na mimba). Pia katika maonesho hayo, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira (Mh.Antony Mavunde, Mb) alitembelea mabanda ya wilaya ya Chemba na kuona shughuli mbalimbali za ufugaji, kilimo n.k.

Zifuatazo ni baadhi ya picha katika maonesho hayo:


No comments:

Post a Comment